Zijue Njia 80+ Halali za Kutengeneza Pesa Mtandaoni 2022.

Kama Ulitumia muda wako mwingi kutafuta kupitia Google,YouTube na Kwingineko juu ya Njia Halali za Kutengeneza Pesa Kupitia Mtandao wa Internet nadhani Utakuwa Umekutana 
na Njia Kama Kuandika Vitabu,Kuanzisha Blogu na YouTube Channel njia Hizi Kwa Vijana Wengi Zimeonekana ndio njia Pekee za Kutengeneza Pesa Mtandaoni.
Kama Wewe ni Mmoja wa Hao Watu Posti Hii Itaenda Kukufungua Macho juu ya Fursa 80+ Kutengeneza Pesa Mtandaoni. Njia za Kutengeneza Pesa Mtandaoni ni Zilezile Dunia Nzima Ila Utofauti Kati ya Nchi na Nchi Unakuja Kwenye Upande wa Njia ya Kuzipata Hizo Pesa Katika Nchi Yako,Sheria za Nchi na  Ujuzi wa Watu Katika Nchi.
Katika Njia Hizo 80+ Kwa Upande Wa Afrika Mashariki Kwa Ujumla. Njia Hizi Kumi(10)Ni Rahisi Kuanza Kwa Kijana(Mteule) Yeyote Mwenye Nia na Kutengeneza Kipato Kupitia Mtandao. 

1.Anzisha Blog
Hii Ni Njia maarufu inayofahamika na wengi na imeweza Kuwafaidisha haswa wale wenye malengo,nia na mbinu sahihi za kuweza kufaidika na njia hizi.Kwa Upande wa Afrika Mashariki
Blogu Zinazolipa Vizuri ni Blog za habari za mastaa,Siasa,Udaku na Michezo,Mahusiano,Muziki,Biashara na Simulizi za Vitabu.Kwa Utafiti wangu ndani ya Miaka  (10) Blog Bora ni Citimuzik,Mabumbe,Millardayo Udakuspecially na Zingine nyingi.

2.Anzisha YouTube Channel
Hii ni njia ambayo nadhani kila Mtanzania Anaifahamu ila siyo Kiunndani zaidi . Kuanzisha YouTube channel si hoja maaana ni kazi ya Dakika moja(1) ila Kuifanya iwe bora na Tayari Kwa  Kuanza safari ya Kuja Kukuingizia Kipato Hiyo ndio hoja ya Msingi. Kuna YouTube Channel zaidi ya 1000+ Tanzania Ambazo Zimehakikiwa na YouTube na Kuingia Katika Mfumo wa Malipo  (Monetization). Ili Kuanzisha YouTube Channel ni Muhimu Kuwa na wazo jipya au lililoboreshwa ili Kumudu Ushaindani Uliopo na Pia Vifaa thabiti Vinavyokidhi Mahitaji Kulingana na aina ya Videos Unazohitaji  Kutengeneza.Kuanzisha YouTube Channel bila Maengo,Bajeti,Ujuzi na Uvumilivu ni Kazi Bure.Moja ya YouTube Channel Bora Tanzania ni MillardAyo(AyoTv),WasafiMedia, Simulizi na Sauti na MpenjaTv

3.Kuandika na Kuuza Vitabu(E-Books/Self Publishing)
Kuna Vitabu vya Kila aina Katika Dunia ya Leo na Mwandishi yeyote Anaweza Kuanza Kazi hii ila Hata Kama Wewe Si Mwandishi Mzuri Unaweza Kumuajiri Mtu Akuandikie.Njia ya Kupata Pesa ni Kuuza E-Books Kwa Njia Zifuatazo .
  • Mitandao ya Kijamii Mfano. Whatsapp,Instagram na Telegram
  • Tovuti Binafsi au Mifumo ya Ununuzi Katika Nchi Husika Mfano.Kwa Tanzania ni  GetValue,SimGazeti 
  • Amazon Self Publishing .(Duniani) Njia Hii ni nyepesi kwa Mtu aliyezoea Kuandika Vizuri Mfano wa Waandishi Wanaofanya hii njia ni Denis Mpagaze,Getrude Mligo,Joel Nanauka na Ernest Benson Makulilo.

4.Kufundisha Mtandaoni
Njia hii ni nyepesi sana endapo Una Ujuzi Uliothibitishwa Kwa Vyeti ambao Unaweza Kuufundisha. Unaweza Ukaanza Kuufundisha Katika Mazingira Halisi,Katika Mitandao ya Kijamii na Kubwa Kuliko
Katika Majukwaa Kama Udemy,Skillshare na Lynda Ambapo Unalipwa Gawio lako Kila Mwezi.Kuanza Njia Hii ni Kuandaa Kozi za Video,Kuzipangilia na Kuziupload Katika Tovuti hizo zihakikiwe na Kusubiri Mapokeo Kwa Wanafunzi ambao Ndio Watakaoamua Ulipwe Kiasi Gani.


5.Kuuza Digital  Assets/ Templates
Digital Asset ni Bidhaa yeyote ya Kidigitali Ambayo Inaweza Kuuzika Bila Mtengenezaji Kupungukiwa Kitu .Katika Kipengele Hiki Digital Assets zinaweza Kuwa Vitabu,Picha Angavu(Stock Photos) Kama Hizi Zinazotumika Katika Blog Hii au Blog ya HabariTech naTanzaniaTech, Beat, Muziki au Website /Blog Theme Template. Pia Kama Wewe ni Graphic Designer Mbobevu Una Uwezo Wa Kuunda Templates za Kila aina Katika Adobe Photoshop au Illustrator basi Njia hii Inakufaa.


6.Kuuza T-Shirt na Bidhaa Zingine za Printing(Print On Demand)

Hii Ni Njia Rahisi Sana hasa Kwa Graphic Designers  Kuanzia Level ya Beginer,Intermediate na Expert. Ambapo wewe Kama Experienced Graphics Designer Unadesign Logo au Sanaa ya Aina Yeyote na Kuiupload Mtandaoni na Kuchagua Ikae Katika Vitu Kama Tshirt,Mito,Makava ya Laptop,Simu,Vikombe na Bidhaa Nyingine Nyingi na Kuziweka Sokoni. Mteja Akinunua Unapata Gawio Lako Tena Kwa Dola,Euro au Pound Kabisa Maana Kupanga ni Kuchagua.  Nadhani Ulishawahi Kununua au Kuvaa Tshirt zenye Maandishi Machache ya Motivation au Yenye Picha ya Ramani ya Afrika yanauzwa Elfu 9-12 .Kama Jibu Lako ni Ndio basi Designer Alishavuta Mkwanja Mrefu Sana.

7.Kujibu Maswali ya Tafiti (Surveys).
Nadhani Ulishawahi Kuona Matangazo ya Mchongo ya Kujaza Schoolarships Kirahisi na Kujaza Kupata Zawadi za Miaka 50 ya Azam au Mlimani City sasa Katika Njia Hii Siyamaanishi Hayo. Namaanisha Njia Halisi Ambayo ni ya Kujibu Maswali Mepesi Kulingana na Uzoefu wako Halisi Ili Kukusaidia Maoresho ya Huduma au Bidhaa na Tovuti hizo ni SurveyJunkie,Swagbucks na Apps Kama Premis.

8.Uuzaji wa Ushiriki(Affiliate Marketing)
Njia hii rahisi Hasa Kwa Mtu Ambaye ana Wafuasi Halisi Katika Mitandao ya Kijamii na Hata Katika Uhalisia Katika Mitandao ya Kijamii na Hata Katika Uhalisia na Njia hii Inawafaa sana Bloggers na YouTube Creators ambapo Unalipwa Kwa Kamisheni ya Link za Bidhaa Mbalimbali Mtandaoni Mteja Akinunua Kupitia Link hiyo Unalipwa na Njia Hii Haina Mtaji.

9.Kazi Huru(Freelancing)
Hii ni njia ya Kuuza Ujuzi Ulionao Kwa Kufanya Kazi Katika Majukwaa ya Kazi Kimataifa ambapo Kazi Hutolewa na Wenye Uwezo wa Kuzifanya Kazi Katika Majukwaa ya Kazi Kimataifa Ambapo Kazi  Hutolewa na Wenye Uwezo wa Kuzifanya Huomba na Kupata Malipo Mara tu ya Kazi Kuishi.Njia hii Inahitaji Mitaji Mitatu tu ambayo ni Ujuzi,Muda na Kifaa cha Internet. Vijana  Wanaofanya Freelancing Kwa Tanzania na Wamefanikiwa Kuwa TopRated Kwa Upande wa Upwork ni Fabian Alex ,Baraka Mafole na Wengine Wengi ambao utazidi kuwafahamu Kupitia Blog Hii ya SwahiliSkills.Freelancing Inabeba Njia zote Zilizopo Katika Orodha Hii Hadi Kufikia Kuwa na Njia 70+Ndani yake

10.Biashara ya Uuzaji na Ununuzi wa Fedha za Kidigitali.
Biashara hii ni Biashara Kubwa Ambayo Imebadili Ndoto za Vijana Wengi Ambao Wametafuta Ujuzi Huu Kwa Muda Mrefu na Kuonesha Juhudi Katika Kufanya Kazi Hii. Vijana  Wengi Walikimbilia Biashara Hii Kichwakichwa na Kuambulia Kupoteza Fedha Nyingi Sana na Wale Walioijua Kwa Kina Wanaendelea Kula Mema Yaliyomo Katika Matunda ya Kidigitali.Vijana Hao Ni Kama Sirjeff Denis na Crainicas.

Je Umegundua Kitu Gani katika Njia Hizi Kumi(80+) Za Leo? Zinahitaji Kualika Mtu? Zina Kiingilio Ukiondoa Forex? Hela Zake Unazipata Kirahisi?
Yote Hayo Utayajua Ndani Ya Blog Hii ya SwahiliSkills.

"Kujua Njia Hizi Bila Kuzitathmini,Kuzielewa na Kuzifanyia Kazi ni Kazi Bure.Suala ni Kuanza Sasa.
Anza Na SwahiliSkills






SUBSCRIBE KATIKA YOUTUBE CHANNEL YETU YA SWAHILISKILLS. UWE KARIBU NA UJUZI HUU ADIMU
Mwandishi. Musa Buzelengule.
@musabuze
Nifollow Instagram @musabuze
         LinkedIn @musabuze
         Twitter @musabuze